Tayari tunahusika katika kupigania haki za watoto wao kwa haki za watoto wote.

imprimer envoyer a un ami
Partager, Share, Compartir
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini Uliokithiri, tarehe 17 mwezi wa 10, 2009, katika Dar es Salaam, Tanzania. Maandalizi yalifanywa na kuadhimishwa na watu wengi wanaoishi katika mazingira magumu katika vitongoji maskini vya Dar es Salaam na sehemu zinazozunguka jiji la Dar es Salaam, na wale wanaopeana bidii zao dhidi ya umaskini uliokithiri.

Takriban watu 300 walikusanyika wakati wa mchana Siku ya Oktoka 17 katika Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama, Dar es Salaam, Tanzania ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini Uliokithiri.

Kwa sababu mwaka huu, tunaunganisha siku hii na sherehe ya miaka 20 ya ukumbusho wa Makubaliano ya Haki za Mtoto. Maadhimisho ya Oktoba 17, 2009 ni nukta ya mkutano huu wa shida za watoto wanaoishi katika ufukara na kutimiza mahitaji katika haki za watoto katika ubia nao.

Maadhimisho ya mwaka huu mambo tuliyoyapa umuhimu ni kuzisalimisha haki za mtoto, hasa haki ya kupata elimu ya msingi, haki ya maendeleo, haki ya kulindwa kutokana na matumizi mabaya na unyanyasaji na haki ya kushiriki katika familia, utamaduni na maisha ya kijamii, kushirikishwa kwa mtoto ina maana kwamba wana haki ya kuelewa maoni yao na hayo maoni yasikilizwe na kutiliwa maanani yanopofaa.

Kupitia shuhuda, nyimbo, mashairi, tamthilia, nk. leo wengi wetu tutaonyesha jinsi gani wako tayari kujumika katika kupigania haki za watoto wao kwa haki za watoto wote.

Angalia nakala chini ya mistari hili.

PDF - 833.6 ko
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini Uliokithiri tarehe 17 mwezi wa 10, 2009 katika Dar es Salaam, Tanzania
photo

Wherever men and women are condemned to live in extreme poverty, human rights are violated.
To come together to ensure that these rights be respected is our solemn duty.

Joseph Wresinski

logo facebook